Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema mageuzi ya kidijitali Tanzania yamesaidia kufikiwa kwa huduma za hitaji hilo ikiwa ni pamoja na elimu na huduma za afya, kuendesha soko shindani na ubunifu, kuboresha maisha ya watu na kukuza ushirikishwaji.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipo muwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan katika mdahalo wa mada isemayo: “Nchi yako iko tayari kujenga uchumi wa kidijitali?” katika jukwaa la Doha Forum lililofanyika Qatar, Desemba 11, 2023.

Amesema, Dunia inabadilika katika suala la matumizi ya kidijitali na Tanzania pamoja na nchi nyingine za Afrika hazipaswi kuachwa nyuma.

Hata hivyo, Dkt. Mwinyi amesema Tanzania inatambua udhamira thabiti wa maono juu ya kuifikisha nchi kufikia malengo ya 4 ya dunia na Mapinduzi ya 5 ya viwanda yanayokuja.

Young Africans yampambania Ranga Chivaviro
Mila: Wanakata Vidole kuifurahisha mizimu