Kocha Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola amewaambia wachezaji wake wasipoteze matumaini baada ya ushindi waliopata wa mabao 2-1 dhidi ya Luton City juzi Jumapili (Desemba 10).

Kikosi cha Guardiola kilipata ushindi kwa mara ya kwanza baada ya kupoteza mechi nne mfululizo na kushushwa kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Guardiola alipata ushindi ikitoka nyuma kwa bao 1-0 dhidi ya Luton City huku presha ikizidi kupanda kwani walikuwa wanahitaji pointi tatu muhimu.

Hata hivyo, Guardiola anaamini alihitaji kuzungumza na wachezaji wake ili kuwatuliza mzuka katika vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mapumziko kabla ya kuibuka na ushindi.

“Tunatakiwa tuonyeshe kitu, niliwaambia walichopaswa kufanya, tujionee huruma? hapana, haya ni maisha na hili ni soka, hata kama Luton ingefunga mabao mawili, tungetoa lawama na kusema hatuna bahati?

“Washambuliaji wanatakiwa kuwa wasumbufu, mabao yanahitajika, safu ya ulinzi inatakiwa kuwa imara. Kawaida kusema Man City sio bora msimu huu, sio mbaya ni vizuri, hebu tuwaonyeshe sisi ni tofauti.

“Tunataka kuendeleza ushindani. Tuna wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa,” alisema Guradiola

Man City ipo nyuma kwa pointi nne dhidi vinara wa Ligi Kuu, Liverpool baada ya Arsenal kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Aston Villa, Jumamosi (Desemba 09), huku Guardiola akisaka ubingwa kwa mara nne ili aweke rekodi.

Wakati huohuo, nyota wa Man City, Jack Grealish, aliongeza: “Nadhani watu wanaongelea Man City kama inapitia kipindi kigumu sana, naamini tumecheza na timu nzuri sana ndo maana matokeo yamekuwa hivyo.”

Kwa upande wa kocha wa Luton Rob Edwards amejivunia kuonyesha ushindani ilipocheza dhidi ya bingwa mtetezi.

“Mechi ilikuwa mkononi kwetu, nilikuwa na hisia nzuri wakati tunaenda kwenye mchezo huo, tumeonyesha heshima kwa Man City, tuliwasumbua sana.”

Kashfa ya rushwa: Mawaziri 15 kutenguliwa
Tanzia, Director Nisher afariki Dunia