Watendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto kote Nchini, wametakiwa kuongeza juhudi katika utoaji wa elimu ili kupunguza vitendo vya ukatili katika jamii.

Akizungumza na watendaji wa Dawati la Jinsia na watoto kutoka Mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar wakati wa kikao cha watendaji hao kinachoendelea Jijini Dodoma, Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimaliwatu, Suzan Kaganda amesema jamii inapaswa kupewa melimu ya kutosha, ili kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia.

Amesema, ”kazi inayofanyika ni kubwa ingawa bado kuna vitendo vya ukatili hivyo watendaji hao wazidishe kutoa elimu pamoja na kubaini na kuzuia vitendo hivyo.”

Aidha, aliwataka watendaji hao kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo kutoa elimu na kazi nyingine ambazo zinatumia rasilimali fedha ili kufanisi kazi za Dawati pia amewataka waliohudhuria kikao hicho kilichoambatana na mafunzo kuhakikisha wanaenda kuwafundisha watendaji na Askari ambao hawakupata fursa ya kufika kwenye mafunzo hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Kimataifa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Renata Mzinga alisema watendaji hao wamejitokeza kwa wingi kuhudhuria kikao hicho na kila Mkoa uliagiza muwakilishi.

Young Africans yamuachia kazi kocha Gamondi
Kocha Mtibwa Sugar aivimbia Young Africans