Kutokana na Wizara ya Afya kuweka jitihada kubwa za uelimishaji jinsi ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko pamoja na usambazaji wa Dawa za kutibu maji Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, Wananchi Wa Kijiji cha Jorodom wamevutiwa na jitihada hizo huku wakiomba ziongezwe zaidi .

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Kijijini hapo Mwenyekiti wa Kijiji hicho na baadhi ya Wananchi wamesema hatua ya Serikali kusambaza mabango ya kuelimisha kuhusu kuzingatia kanuni za afya kujikinga na magonjwa pamoja na usambazaji wake ni nzuri katika kuwajali.

“Hii elimu ni nzuri sana, maana maana inatupa mwongozo tufanye nini pia kitendo cha kutibu maji mnajali usalama wetu tunataka vidonge zaidi na zaidi,“ alisema mmoja wa wananchi hao.

Jorodom ni Kijiji cha kwanza kuathiriwa na maji ya mafuriko yaliyoambatana na maporoko ya tope, magogo na mawe hali iliyosababisha vifo na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya maji, nyumba na vitu mbalimbali.

Scott MCTominay afunguka jambo Man Utd
SMZ yapongezwa maboresho Uwanja wa Amaan