Uongozi wa Manchester United unafikiria kumtoa winga wao, Jadon Sancho, kama sehemu ya ofa kwenda FC Barcelona ili kuipata huduma ya winga wa timu hiyo Raphinha, wakati wa dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Sancho mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akihusishwa na timu nyingi tangu kuibuka taarifa za kuondoka baada ya kupishana kauli na kocha wake Erik Ten Hag.

Tangu dirisha lililopita Raphinha mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akitajwa ataondoka Barcelona lakini ni kwa kuuzwa ili kuipa timu hiyo pesa itakazotumia kufanya usajili wa kuendesha timu.

Hata hivyo, Raphinha mwenyewe mara kadhaa amekuwa akipinga suala hilo na kusisitiza bado anahitaji kuendelea kusalia Barca.

Kwa sasa Raphinha ni mmoja kati mastaa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha wababe hao kutoka Nou Camp na tangu kuanza kwa msimu amecheza mechi 15 za michuano yote na kutoa asisti tano.

Wakati Sancho ambaye kwa sasa anatanya mazoezi na kikosi cha akiba, msimu huu amecheza mechi tatu za Ligi Kuu England.

Maxi: Young Africans inakwenda Robo Fainali
Mtambo wa kutibu Magonjwa zaidi ya 10 wazinduliwa