Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Anamringi Macha hii leo Desemba 13, 2023 ametoa salaam za CCM kwa Viongozi vijana Wanawake kutoka nchi 16 za Afrika, wanaohudhuria Mkutano wa Mwaka wa Asasi ya Kiraia wa Young Women of Africa (YWOA), toka katika Vyama Tawala za nchi hizo.

Mkutano huo, unaoendelea katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, iliyoko Kibaha, mkoani Pwani, unafanyika sambamba na mafunzo na mijadala ya masuala anuai, yanayowahusu Wanawake na Uongozi katika nyanja mbalimbali kwenye jamii za Afrika na dunia kwa ujumla.

Aidha, Mkutano huo pia umeweka maazimio yatayakochangia mustakabali wa jamii zilizo bora zaidi kwa kila mmoja, ambapo mapema hapo jana Desemba 12, 2023 Wanawake wenye sifa za kuwa Viongozi, walitakiwa kuanza maandalizi ya kugombea nafasi mbalimbali katika chaguzi za Serikali za Mitaa mwakani na uchaguzi Mkuu wa 2025, ili walisaidie Taifa kupiga hatua za maendeleo.

Wito huo, ulitolewa na Katibu Mtendaji wa kanda ya Afrika Mashariki wa Pan African Women Organization – PAWO, Dkt. Suzan Kolimba wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu huo, uliohusisha Viongozi Wanawake Vijana wanaotoka nchi 20, ikiwemo Kenya, Tanzania, Namibia, Zimbabwe, Rwanda, afrika ya kusini, Angola, Zambia, Madagaska, Uganda na Swaziland.

Man City kumsaka mbadala wa Haaland
Aweso ataka weledi, viwango utekelezaji miradi ya Maji