Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Miguel Angel Gamondi, ameweka wazi kuwa kikosi chake kinakuja na mpango kazi mpya kwa ajili ya kuhakikisha kinapata matokeo kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Kauli hiyo ya kishujaa imetolewa na kocha huyo kutoka nchini Argentina, huku kikosi chake kikiwa katika maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, utakaopigwa keshokutwa Jumamosi (Desemba 16), katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Wakati maandalizi ya mchezo huo yakiendelea, upande wea Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Hatua ya Makundi baada ya kucheza mechi tatu, Young Africans imeambulia pointi mbili tu, na safu ya ushambuliaji imefanikiwa kutupia mabao mawili. Kwa upande wa safu ya ulinzi inayoongozwa na Dickson Job iliruhusu mabao matano.

Kocha huyo amesema kuwa kinachotakiwa katika mashindano ya kimataifa ni utulivu kwenye kutimiza majukumu na kucheza kwa kujiamini.

“Ninawapongeza wachezaji kwa namna ambavyo wanajituma katika mechi zetu. Kikubwa kwenye mashindano ya kimataifa ni kuwa watulivu na kupunguza makosa kwenye mchezo husika.

“Tuna kazi kubwa kupata matokeo uwanjani inawezekana kutokana na uwezo wa wachezaji waliopo, lakini bado tunapaswa kupunguza makosa kwenye eneo la uwanja na haya yote tutafanyia kazi eneo la mazoezi,” amesema Gamondi.

Maslahi yamuondoa Kitambi Namungo
Mambo matatu kuibeba Simba SC Ligi Kuu