Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kazi ,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wameendelea kuratibu ajira za wageni ambapo jumla ya maombi 8,392 ya Vibali vya Kazi yamepokelewa na kufanyiwa kazi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi ameongeza kuwa kati ya maombi hayo, 7,729 yamekubaliwa na maombi 82 yamekataliwa kutokana na kutokidhi vigezo vya kisheria.

Amesema, wataendelea kuchukua hatua kwa waajiri wanaothibitika kukiuka Sheria za kazi ambapo jumla ya Waajiri 199 wamepatiwa amri tekelezi ya kutakiwa kurekebisha mapungufu ya kisheria yaliyobainika na waajiri 2 wamefikishwa Mahakamani.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi.

“Tunajua kila sehemu kuna sheria na taratibu zake ,hivyo hatutaacha kuchukua hatua pale ambapo tunaona ukiukwaji wa sheria unaenda ndivyo sivyo, lazima Waajiri wawe na nidhamu kwa waajiriwa na waajiriwa pia wawe na nidhamu,” amesema

Aidha ameongeza kuwa, “kama ambavyo nimesema mwanzo teyari Waajiri wawili wamefikishwa mahakamani kwaajili ya mashtaka kuanza kusomwa, hivyo mnatakiwa tu mtambue Ukiukwaji wa sheria ni kosa kisheria”.Amesema Katambi

Hata hivyo, Katambi ameongeza kuwa wanaendelea kuimarisha mahusiano na ushirikiano baina ya wadau na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kazi ,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na kusajili Mikataba ya Hali Bora inaoyoingiwa kupitiwa Majadiliano ya Pamoja kati ya waajiri na Vyama vya Wafanyakazi ambapo jumla ya Mikataba 49 imesajiliwa.

Ziara: Mahundi akagua miradi ya Maji Mtwara
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 15, 2023