Afarah Suleiman, Hanang – Manyara.

Katika kuunga mkono juhudi za Serikali, kusaidia waathiirika wa mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya tope, mawe na maji katika mji wa Katesh Wilayani Hanang Mkoani Manyara, Shirika lisilo la kiserikali la AMO Foundation limetoa misaada kwa waathirika wa Mafuriko.

Afisa Mahusiano wa Shirika hilo, Ramadhan Rajabu amesema wamefikisha msaada huo kwa kumuwakilisha Mkurugenzi wao, Amina Said na kutoa unga wa sembe Tani tatu, Maharage tani Moja pamoja na mafuta ya kupikia.

Akipokea msaada huo Naibu Waziri wa Ujenzi, Geofrey Kasekenya amewaomba wadau wenye nia ya kuendelea kutoa misaada ya hali na mali wilayani Hanang kwaajili ya waathirika wa tope kuweka kipaumbele vifaa vya ujenzi, ili kusaidia kutimiza lengo na takwa la Rais Samia Suluhu Hassan la kuwajengea makazi waathirika.

Awali akizungumza Kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa AMO Foundation, Amina Said alisema katika juhudi za kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kuwasaidia waathiirika hao, anaahaidi atafika mji wa katesh Desemba 27, 2023 ili kutoa misaada ya vifaa vya ujenzi vitakavyosaidia ujenzi wa makazi ya waathiiriwa.

Mchengerwa awaonya wakwamishaji wa miradi Kagera
Serikali kukamilisha sehemu ya mradi ujenzi Nyumba 5,000