Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekabidhiwa mfano wa ramani ya mji mpya wa biashara na uwekezaji, Nyamanzi Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi .

Akipokea ramani hiyo Ikulu, Zanzibar kutoka kwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Omar Said Shaaban Dkt. Mwinyi amepongeza hatua za awali zilizofikiwa na wazo la ujenzi wa mji huo.

Kwa uoande wake Waziri Shaaban alisema ujenzi wa mji huo wa kisasa utajumuisha ikiwemo ukumbi mkubwa wa mikutano wa kisasa wa kimataifa, hoteli kubwa za kisasa zenye hadhi ya nyota tano.

Aidha, kutakuwa pia na ujenzi wa eneo la kisasa la biashara litakalohusisha maduka makubwa, Makaazi ya kisasa ya wananchi, ujenzi wa hospitali ya kisasa pamoja na kuwekwa viwanja vya michezo.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 17, 2023
Mfumo kubaini makosa Barabarani kutumiwa kikamilifu