Wananchi katika kijiji cha Hangomba Wilayani Mbozi Mkoani Songwe, wametakiwa kuachana na imani potofu za kishirikina ikiwemo ramli chonganishi pamoja na unywaji wa pombe uliopindukia.

Kauli hiyo, imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Theopista Mallya wakati akizungumza na wanakijiji hao kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu madhara ya ushirikina, kujichukulia sheria mkononi na vitendo vingine vya kikatili

Amesema, unywaji Pombe kupindukia umekuwa na matokeo hasi kwenye jamii ambapo asilimia kubwa ya watu waliojiingiza kwenye matendo hayo wamekuwa wakiishia kwenye mikono ya sheria baada ya kutenda uovu kinyume na sheria, kanuni na taratibu za nchi.

“Unapo kunywa pombe kupita kiasi au unapokuwa mtu wa kuamini imani potofu za kishirikina na ramli chonganishi ni lazima utafanya vitendo viovu, kinachotakiwa ni kumrudia Mwenyezi Mungu na kuacha kabisa vitendo hivyo ili kuepuka kuingia kwenye mkono wa sheria,” alisema Kamanda Mallya.

Hata hivyo, ametoa wito kwa Wanakijiji hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, ili kudhibiti matukio ya mauaji yanayotokana na imani za kishirikina na uhalifu mwingine kwenye maeneo yao.

Zaidi ya watu milioni kutoshiriki uchaguzi DRC
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 18, 2023