Miamba ya soka nchini Italia ‘Juventus’ imezungumza na Manchester City kuhusu Kalvin Phillips wakati wanaangalia kuongeza kiungo wa kati ifikapo Januari 2024, lakini wanatafuta chaguzi kadhaa katika hatua hii, vyanzo vimeiambia 90min.

City wameweka wazi kwa Phillips anaweza kuondoka Januari 2024 iwe kwa uhamisho wa kudumu au kwa mkopo.

90min ilifichua mapema mwaka huu, Phillips alikuwa akijitolea hadi Krismasi kujaribu kumshawishi Pep Guardiola, alikuwa na jukumu la kuichezea City.

Hata hivyo, hilo halijatimia na mchezaji huyo wa zamani wa Leeds United sasa yuko tayari Kwa muda mrefu. Juventus wamekuwa wakimtaka nyota huyo wa kimataifa wa England.

Wanatazamia kuleta kiungo wa kati Januari 2024, na wamezungumza na City kuhusu maelezo ya dili la Phillips.

Timu hiyo ya Serie A ingependelea kumchukua Phillips kwa mkopo wa awali na City wako tayari kufanya hivyo.

Man City ingependa kifungu cha lazima cha ununUuzi katika mpango huo, lakini wako wazi kwa chaguo ambalo litakuwa na vichochezi vya kuifanya iwe ya kudumu.

Huenda Juve ina kiasi kidogo cha fedha kuelekea Januari 2024 kama ilivyo kwa klabu nyingi, ingawa uwezekano wa kusimamishwa kwa Paul Pogba kunaweza kusaidia.

Zaidi ya hayo, Juve wanaangalia malengo mengine na Mkurugenzi wa Michezo, Cristiano Giuntoli, amekuwa akifanya kazi yake juu ya chaguzi nyingi.

Makala: Usiwaamini Viumbe hawa 10, ni hatari
Baraza aongeza mzuka Dodoma Jiji