Licha ya ushindi wa mabao 2-0 ambao Simba wameupata dhidi ya Wydad Casablanca lakini Kocha Mkuu wa timu hiyo, Abdelhak Benchikha amesema kuwa bado timu yake haijafika asilimia mia kiuchezaji kama ambavyo anahitaji.

Kocha huyo tangu atue Simba SC amepoteza mchezo mmoja tu, dhidi ya Wydad Casablanca huku pia akiipa ushindi katika mchezo wa marudiano wa Kundi B, Ligi ya Mabingwa Afrika na kuipeleka Simba SC nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi hilo.

Kocha huyo kutoka nchini Algeria amesema kuwa “Bado hatujafikia pale ambapo tunapahitaji, tunafanyia kazi kuona timu inakuwa bora kwa asilimia kubwa zaidi ya sasa, tunashukuru kuwa tumepata matokeo mazuri.

Tunatakiwa kuendelea kufanyia kazi yale mapungufu yote ambayo yanajitokeza kwa sasa, wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mapambano na sisi tutahakikisha kuwa tunawapa mbinu nzuri zaidi.

“Bado tupo kwenye mipango ya kuiimarisha timu, kuna madirisha yajayo ya usajili, naamini kila kitu kitakuwa sawa, lengo kubwa ni kufika pale ambapo tunapahitaji, mashabiki, viongozi na wachezaji tunatakiwa kuwa pamoja ili tufike tulipopahitaji.” amesema Benchikha.

Polisi watoa tamko tuhuma utesaji wa raia
JKT Tanzania kuingia sokoni Dirisha Dogo