Johansen Buberwa, Missenyi – Kagera.

Wakala wa Misitu Tanzania – TFS, Wilayani Misenyi Mkoani Kagera wametoa msaada wa madawati 90 yenye thamani ya shilingi milioni tano, katika shule mbili za Sekondari za Ruzinga na Bungandika, ili upunguza uhaba wa madawati na kuendeleza mshikamano baina ya taasisi na jamii.

Akizungumza wakati akikabidhi Madawati hayo, Mhifadhi Misitu Wilaya Misenyi, Mrisho Juma amesema Madawati hayo pia yatasaidia kuwapa ufanisi Wanafunzi na kuongeza ufaulu wa elimu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Misenyi, Kanali Hamis Mayamba amesema Madawati hayo yatumike kwa malengo kama ilivyo pangwa.

Nao Walimu Wakuu wa shule hizo wamesema awali kulikuepo na changamoto ya utoro na Wanafunzi kugombania Viti na meza, hivyo Madawati hayo yatasaidia kuongeza ufanisi.

  • CODEPATA waifikia jamii maafa ya mafuriko Hanang’

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 23, 2023
CODEPATA waifikia jamii maafa ya mafuriko Hanang'