Afarah Suleiman, Hanang’ – Manyara.
Kampuni ya uzalishaji wa mabati – ALAF, imetoa msaada wa mabati 2000 yenye thamani ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Hanang’ walioathiriwa na janga la maporomoko ya udongo, matope na mawe yaliyotokea Desemba 3, 2023.
Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya uongozi, Afisa Mahusiano wa ALAF, Teddy Mmasi amesema Kampuni hiyo inaungana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwapa pole na kuchangia kiasi hicho cha Mabati, ili kusaidia kujenga upya makazi yao.
Msaada huo, umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Hanang’n Janeth Mayanja ambaye ameishukuru kampuni ya ALAF Kwa namna walivyoguswa na changamoto za wananchi wa Hanang na kuwahakikishi wadau hao na wadau wengine ambao watajitokeza kuwa itawafikia walengwa.
Aidha misaada mbalimbali imendelea kuwasili katika wilaya hiyo ikiweo vyakula,mavazi pamoja na vifaa vya ujenzi wa nyumba za waathiirika hao wa maporomoko yaliyosababisha vifo na majeruhi.