Johansen Buberwa – Kagera.
Serikali imeweka Bago la Chuo Kikuu cha Nelson Mandela na kupanda miti, ikiwa ni ishara ya kuanza ujenzi wa chuo hicho kweye Kijiji cha Kyamalange kata ya Rubafu iliyopo Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera.
Akizungumza wakati wa kuweka bango hilo, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajath Fatma Mwasa amesema wazo la kujenga Campas ya chuo hicho limekuja kutokana na ufugaji wa vizimba unaotarajiwa kujengwa kwenye kata ya Rubafu.
Amesema, Wananchi wa kijiji cha Kyamalange pamoja naongozi wa Halmashari hiyo kwa kushirikiana na wanakijiji wametoa ekari 300 na ujenzi huo utagharimu Dola za Kimarekani milioni moja kwa uratibu wa mfuko wa Maendeleo Tanzania – TACTCI.
Hata hivyo, amesema vipaumbele vya mradi huo ni uanzishwaji wa ufugaji wa Samaki kwa Vizimba, uanzishwaji wa kituo cha utafiti wa mazao ya ziwani kupitia chuo cha Nelson Mandela na uwezeshwaji wa Wananchi katika shughuli za Kilimo cha kujikimu.
Kwa upande wake Prof. Ernest Mbega wa chuo Kikuu Nelson Mandela Campus ya Arusha, amesema ajenda ya umoja wa Afrika ilibebwa na mwasisi wa Taifa la Afrika ya Kusini, Hayati Nelson Mandela ambaye alitaka Afrika ijitegemee kiteknolojia ambapo mpaka sasa tayari vimejengwa vyuo vitatu Africa ikiwemo cha Arusha, Naigeria, Bukinafaso na kingine kitajengwa Afrika Kusini au Zimbabwe.
Awali, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt. Jasson Rweikiza aliishukuru Serikali kwa mipango mizuri inayoendelea kutekeleza kwa Taifa hilo kwa maana inasaidia kuleta Maendeleo kwa Mkoa wa Kagera na kuomba Msaada wa kiuchumi.
Rweikiza ameomba pia kupunguzwa kwa bei ya Simenti, Mafuta ya Petroli pamoja na kodi ya VAT kwa kanda ya ziwa pamoja na Mkoa huo, hali itakayosaida kupata maendeleo kwa haraka tofauti na maeneo mengine ambayo gharama zake ni zakawaida.