Klabu ya Manchester United imeungana na Manchester City na Liverpool kwenye mchakato wa kuiwania huduma ya kiungo wa Mabingwa wea Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Joshua Kimmich, kuelekea dirisha lijalo.

Kimmich mwenye umri wa miaka 28, ni mmoja kati ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Munich, anadaiwa kuwa hana mpango wa kuondoka Januari 2024, na badala yake atasubiri hadi mwisho wa msimu huu.

Timu nyingi zimevutiwa na staa huyu ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2025.

Awali, FC Barcelona na Manchester City ndio zilionekana kuwa na uhitaji zaidi wa staa huyu lakini hivi karibuni Man United inadaiwa kuanza mazungumzo na wakala wake kuangalia uwezekano wa kumsajili.

Kimmich, ambaye alijunga na Bayern akitokea RB Leipzig mwaka 2015, kiujumla amecheza mechi 367, akifunga mabao 41 na kutoa asisti 100.

Man United inatarajiwa kuingia sokoni kusaka majembe baada ya Sir Jim Ratcliffe kukamilisha ununUzi wa asilimia 25 za hisa za klabu hiyo.

Kauli ya Lusajo yaibua minong'ono
Mabasi matano yazuiwa kuendelea na safari