Kiungo Mshambuliaji wa Namungo FC, Shiza Kichuya huenda akaachana na Klabu hiyo katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili, huku klabu ya JKT Tanzania ikipewa nafasi kubwa ya kumsajiuli.
Taarifa zinaeleza kuwa tayari Uongozi wa JKT Tanzania umeshaanza mchakato wa kumsajili Kichuya, na dalili zinaonesha kila kitu kuhusiana na mchezaji huyo kinaenda sawa na muda wowote anaweza akasaini.
Japokuwa haijawekwa wazi ni mkataba wa muda gani ambao Kichuya alibakiza na Namungo FC, lakini inaelezwa taratibu zote zinafuatwa ili kuhakikisha wanainasa saini yake.
“Kichuya ni mchezaji mzuri na ana uwezo wa kutumia miguu miwili kucheza na ndio maana mwepesi wa kucheka na yavu anapopata fursa hiyo,” amesema kiongozi huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe.
Tunazungumza na viongozi wa Namungo FC kuona hilo jambo linakwenda kwa kuzingatia taratibu zinazotakiwa, ila ni asilimia kubwa winga huyo anaweza akajiunga na sisi.”
Kichuya alipata umarufu mkubwa baada ya kuichezea Simba SC miaka kadhaa iliyopita, kutokana na kiwango chake alichokuwa akikionyesha ikiwemo kuifunga Young Africans, kama bahati aliyonayo Mshambuliaji wa KMC, Waziri Junior kuwafunga Wanamsimbazi mara nyingi.