Uongozi wa Singida Fountain Gate unatajwa kuipikua Young Africans katika vita ya usajili wa kiungo Mshambuliaji kutoka DR Congo Manu Labota Bola, akitokea FC Lupopo.

Young Africans ilikuwa na hesabu za kumsajili Labota ikitangulia kuonyesha nia ya kumsajili kabla ya kupunguza kasi kidogo kuwania saini yake.

Singida Fountain Gate ilicheza na akili kubwa kwa kumpiga hesabu kali kwa kuamua kumpandia ndege Labota na kwenda kumaliza dili hilo kimyakimya, huko huko kwao jijini Lubumbashi.

Labota bado alikuwa na mkataba na FC Lupopo ambapo Singida Fountain Gate ikatumia nguvu ya kigogo wao mmoja kumaliza dili hilo kwa kuwasiliana na Rais wa klabu hiyo Jacques Kyabula Katwe ambaye pia ni gavana wa jiji hilo.

Winga huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuja kuitumikia Singida Fountain Gate baada ya kuwa na miaka mitatu ndani ya Lupopo.

Imefahamika kuwa Uongozi wa Singida Fountain Gate ilimsafirisha mmoja wa vigogo wa timu hiyo Ramadhan Nswazurimo kumalizia usajili huo na wakati wowote wiki hii Bola atatua nchini kuja kuanza maisha mapya.

Taarifa kutoka FC Lupopo zinasema Singida Fountain Gate imelazimika kutumia zaidi ya Sh250 milioni kukamilisha dili hilo la Labota baada ya Lupopo kuwa na hesabu za kutaka kumuuza Afrika Kusini.

Chasambi kutambulishwa Mapinduzi CUP 2024
Kichuya kuibukia JKT Tanzania