Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdellhak Benchikha amesema kuwa anakwenda kutumia mashindano ya Kombe la Mapinduzi kuimarisha viwango vya wachezaji wake, kabla kurejea kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Kwenye michuano hiyo ambayo itaanza kesho Alhamis (Desemba 28) Simba SC imepangwa Kundi B pamoja na APR, Singida FG na JKU, huku mchezo wa fainali ukitarajiwa kufanyika Januari 13, Uwanja wa Amaan, Kisiwani Unguja.

Msimu uliopita Mlandege ilibeba taji hilo kwa kuifunga Singida kwa mabao 2-1, huu ni msimu wa 18 wa michuano hiyo tangu mwaka 2007, huku Azam FC ikiwa ni timu iliyoshinda makombe mengi ikibeba mara tano, ikifuatiwa na Simba SC manne.

Kocha Benchikha amesema bado anaendelea kukisuka kikosi chake hivyo kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Mapinduzi ni nafasi ya kuendelea kujiimarisha zaidi na kutoa nafasi kwa wachezaji ambao hawajapata nafasi kuonesha viwango vyao.

“Tunaenda kwenye mashindano haya lengo likiwa ni kwenda kupambana na kutwaa ubingwa lakini pia kuimarisha kikosi changu kwa kuendelea kupunguza makosa yanayo tugharimu.

“Nitaenda kuwatumia wachezaji ambao hawajaitwa kwenye timu za taifa lakini pia wale ambao hawajapata nafasi ya kuonekana katika michezo kadhaa ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika ni wakati wao wa kuonesha ubora wao,” amesema Benhikha.

Katika michuano hiyo Kundi A lina timu za Azam FC, Vital’ O, Chipukizi na Mlandege wakati Kundi’C ni Young Africans, Jamhuri, KVZ na Jamus

Bingwa wa Kombe la Mapinduzi 2024, atachukua kitita cha Sh milioni 100 na mshindi wa pili ni Sh milioni milioni 70.

Mchezo wa ufunguzi utakuwa kati ya mabingwa watetezi Mlandege dhidi Azam FC, Uwanja wa Amaan Kisiwani Unguja, saa 10:00 jioni.

Makala: Ukweli kuhusu ujenzi wa Hotel kwenye Sayari ya Mars
Azam FC: Moto utaendelea kuwaka Ligi Kuu