Beki kutoka nchini Ufaransa Raphael Varane ameripotiwa kufanya uamuzi juu ya uwezekano wa kuhamia Saudi Arabia baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha Manchester United.

Beki huyo ametatizika kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara Old Trafford msimu huu, ameanza mara tano tu kwenye Ligi Kuu England, huku mastaa kama Harry Maguire, Victor Lindelof na Jonny Evans, mara nyingi wakianza mbele ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.

Hii imesababisha uvumi anaweza kuondoka katika klabu hiyo, huku ikiripotiwa anatakiwa Saudi Arabia pamoja na klabu yake ya zamani ya Real Madrid, ambapo anaweza kuchukua nafasi ya David Alaba ambaye ni majeruhi.

Kuhamia katika Saudi Pro League kunaweza kumfanya kuungana tena na mchezaji mwenzake wa zamani wa Los Blancos, Karim Benzema.

Gazeti la LEquipe limeripoti wawakilishi wa Varane wamedai kuhamia Saudi Arabia au Qatar ni’mpango wao’.

Varane aliwahi kutangaza atamaliza soka lake aidha Real Madrid, Manchester United au Lens, ambapo alianza maisha yake ya soka.

Mfaransa huyo ana uhusiano mkubwa na wababe hao wa Hispania, akiweka uhusiano na wachezaji na wasimamizi ambao amefanya nao kazi, na hata ku- weka nyumba yake huko.

Hata hivyo, hakujawa na mawasiliano kati ya klabu na mchezaji kuhusu uhamisho wa dirisha lijalo la Januari.

Inadaiwa Varane hapendi kubadili klabu katikati ya msimu, lakini anajua hali yake ya sasa ndani ya Manchester United haiwezi kuongezwa kwa zaidi ya msimu mmoja.

Mail Sport iliripoti wiki iliyopita Mkurugenzi wa Soka wa Manchester United, John Murtough, alisafiri kwa ndege hadi Saudi Arabia ili kujadili uwezekano wa kuondoka kwa Varane, Jadon Sancho, Casemiro, Anthony Martial na wachezaji wengine.

Murtough anafahamika kuondoka Saudi Arabia bila kufikia makubaliano juu ya uhamisho wowote, lakini alianzisha uhusiano mpya muhimu kwa United na mazungumzo zaidi yamepangwa.

Varane alijiunga na United akitokea Real Madrid msimu wa joto wa 2021 na kuunda ushirikiano mzuri na Lisandro Martinez msimu uliopita.

Hata hivyo, huku Martinez akikosa mechi nyingi za sasa kutokana na jeralha, Ten Hag hajabaki na Mfaransa huyo ambaye mara nyingi amekuwa chaguo la nne au la tano katika miezi ya mwanzo ya msimu.

Mkataba wa Varane na timu hiyo ya Old Trafford unamalizika ifikapo mwaka 2025, lakini kuna uwezekano mkubwa kutokana na matatizo ya United msimu huu, na kukosa muda wa kucheza kwa beki huyo klabuni hapo majira ya joto kijacho.

Mahakama yafuta kesi ya Gekul, rufaa kukatwa
Steven Gerrard hali mbaya Saudi Arabia