Hatimaye nyota wa kimatifa wa Tanzania aliyekuwa akikipiga katika Klabu ya JS Kabylie ya nchini Algeria, Simon Msuva, amefunguka suala la kuhusishwa kujiunga na klabu za Simba SC na Young Africans.

Kwa sasa Msuva hana timu baada ya kuachana na Klabu ya JS Kabylie ya Algeria ambayo alijiunga nayo Desemba 19, 2023, akitokea Al-Qadsiah ya Saudi Arabia, ambayo ilimsajili tangu Julai 24, 2022 akitokea Wydad AC ya Morocco.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa Young Africans imekuwa ikifanya mchakato wa kumtaka kumsajili Msuva kwa mkataba mfupi ili awasaidie kwenye michuano ya kimataifa.

Msuva ameweka wazi kuwa, baada ya kuachana na JS Kabylie kwa maelewano ya pande mbili, sasa haangalii nyuma na hana mpango wa kucheza Tanzania.

Ameongeza siku si nyingi atatoa taarifa za nchỉ gani ataenda na hana mpango wa kurejea nyumbani kucheza iwe Young Africans au Simba SC, anachoangalia kwa sasa ni kujikita kwenye soka la kulipwa kutokana na ukubwa wa wasifu yake na muda ukifika basi atarejea Tanzania kumalizia soka lake.

Kwa sasa naweza kuweka wazi kabisa kuwa maisha ya Algeria yameshapita kwani nimemalizana nao vizuri tu kwa maana ya pande zote mbili tumekubaliana, ila nafahamu wazi kabisa kuwa kwa sasa kila mtu ataongea lake ila mimi najua nini nafanya. Si unajua Tanzania yetu.

Ninachoweza kusema nina CV kubwa hivyo siwezi kukosa timu kwa uwezo wa Mungu nitapata tu na nitakwambia mapema tu wapi naelekea ila siwezi kurudi kucheza nyumbani mapema hii,” amesema Msuva.

Ahmed Ally: Chama ataondoka Simba SC kwa heshima
Kifaru: Tutasasajili kwa kishindo Dirisha Dogo