Kijana wa Rais wa Liberia George Weah anayetarajia kuondoka madarakani, Tim Weah atacheza mechi yake ya kwanza akiwa na Juventus baada ya siku 63 watakapocheza dhidi ya AS Roma keshokutwa Jumamosi (Desemba 30).

Kwa mujibu wa Gazzetta dello Sport, baada ya kuonyesha kiwango bora akitokea benchi dhidi ya Frosinone, atachaguliwa kikosi cha kwanza na kocha Massimiliano Allegri kwa ajili ya mechi hiyo ya Serie A.

Nyota huyo ambaye anaichezea timu ya taifa ya Marekani, walionyesha ushirikiano mzuri kati yake na Weston McKennie katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Frosinone na kumshawishi Allegri.

Weah hajacheza kikosi cha kwanza tangu Oktoba mwaka huu, alipotemwa dhidi ya Hellas Verona kutokana na majeraha.

Baada ya miezi miwili ya kukaa nje ya dimba amerejea Desemba 15 kwenye mechi dhidi ya Genoa kabla ya mechi ya wikiendi iliyopita walipocheza dhidi ya Frosinone.

Baada ya kucheza mechi mbili mfululizo, anatarajiwa kucheza mechi ya kwanza tangu alipokumbwa na majanga ya majeruhi.

Weah alikipiga PSG mwaka 2018 sambamba na Neymar na Kylian Mbappe, na kufunga mabao mawili katika mechi sita alizojumnuishwa kikosini.

Vibibi kizee wa Turin watacheza dhidi ya kikosi cha Jose Mourinho katika mpambano mkali wva Serie A unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki.

Timu ya Weah imneipita Roma kwa tofauti ya pointi 12 kwenye msimamo wa Serie A, na ushindi utapunguza uwiano wa pointi na vinara wa ligi Inter Milan.

 

Benchikha abadili mpango usajili Simba SC
Makonda ataka ushirikiano endelevu Serikali, Viongozi wa Dini