SIR Jim Ratcliffe hataruhusiwa kuwakosoa wawekezaji wenzake wa Manchester United, Avram Joel Glazer kama sehemu ya makubaliano ya dili lake baada ya kununua hisa.

Klabu ya Man United imethibitisha rasmi bilionea huyo kutoka England, amenunua hisa kwa asilimia 25 iliyogharimu Pauni 1.25 Bilioni.

Kama sehemu ya dili hilo, Ratcliffe na familia ya Glazer wamekubaliana kwamba hawatakosoana hadharani kwa mujibu wa ripoti.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Gazeti la British, nyaraka ya makubaliano imetumwa hadi New York, Marekani kwa familia ya Glazer ikielezea makubaliano mbalimbali waliyowekeana.

Makubalino hayo yaliandikwa hivi: “Hujumuisha shambulio la hadharani, kukosoa, au kudharau wawekezaji (familia ya Glazers), kampuni (Man United) au washirika wao.”

Dokumenti zimethibitisha kwamba watu wawili wa Ratcliffe kwenye Kampuni ya INEOS, Sir Dave Brailsford na Jean Claude Blanc, watajiunga na bodi ya Man United.

Ingawa uwekezaji wa Ratcliffe bado haujaidhinishwa na Ligi Kuu England, taarifa imeripoti Man Unted inatakiwa kuwasiliana na INEOS kwa ajili ya masuala yote ya usajili wa wachezaji dirisha dogo Januari 2024.

Mkataba wa Ratcliffe italazimika kutolewa wazi na Ligi Kuu England, pamoja na wanahisa wa daraja A wa klabu hiyo.

Mara tu mpango huo utakapokamilika, familia ya Glazer itapata faida ya kutengeneza pesa Pauni 715 milioni baada ya kumuuzia hisa Ratcliffe.

Mtego mzito Young Africans
Chama awekwa sokoni kwa Dola 300,000