Mataikun wa Saudi Arabia wameripotiwa kuanza tena mazungumzo na wakala wa kiungo wa Manchester City, Kevin de Bruyne ili kuipata saini ya kiungo huyo katika dirisha hili ama lijalo.

Waarabu hawa walijaribu kutaka kumsajili staa huyu katika dirisha lililopita lakini ilishindikana baada ya Man City kudaiwa kukataa kumuuza.

Hata hivyo, katika kipindi hiki, mabosi wa Man Ciy wameonyesha nia ya kutaka kumpiga bei kwa sababu amekuwa akipata majeraha ya mara kwa mara, ambayo yamesababisha awe nje ya uwanja kwa muda mrefu hususan kwa msimu huu.

De Bruyne staa wa kimataifa wa Ubelgiji ambaye mkataba wake Man City unatarajiwa kumalizika mwaka 2025, msimu huu amecheza mechi mbili tu na kutoa asisti moja hiyo yote ikichangiwa na majeraha aliyokuwa anauguza.

Fundi huyu anapokea mshahara wa Pauni 400,000 kwa juma na kwa mujibu wa taarifa ni kwamba huenda akienda Saudia atapokea mshahara mnono zaidi. Unadaiwa unaweza kuwa mara mbili ya huu wa sasa.

Makala: Ufahamu Mmea unaokula Wadudu, Pombe yahusika
Simba SC, APR kumalizana Zanzibar