Madereva wa Pikipiki maarufu kama Bodaboda huko Malindi Nchini Kenya, wameishtaki Serikali ya Rais William Ruto wakidai imeshindwa kuwashirikisha katika mipango yake.
Madereva hao, wamesema mwaka 2022 Kenya Kwanza iliendesha kampeni ya kuwainua bodaboda na Mama Mboga na bado inanadiwa kuwa wao (bodaboda) na Mama Mboga wanahusishwa jambo ambalo wanadai si kweli.
Wanasema, wanaendelea kuteseka na kupata hasara katika Sekta hiyo kutokana na gharama za juu za maisha na raia wengi kukosa imani na Serikali juu ya uteremshaji wa gharama ya maisha.
“Hii haijakaa sawa Kenya kwanza wakuje watuambie ni gani tunashirikishwa, wanadai mama mboga na bodaboda lakini tunajiuliwa ni wa wawapi mbona hapa hamna? walihoji.