Mshambuliaji wa Singida Fountain Gate Habib Kyombo amesema kazi ndio imeanza kwa vile hatua waliyofuzu ya Robo Fainali, Kombe la Mapinduzi ndiko kwenye kazi na anajivunia kiwango alichonacho kwa sasa.
Singida inayonolewa na Thabo Senong, inashika nafasi ya kwanza katika msimamo wa Kundi B ikiwa imemaliza mechi tatu, huku msimamo huo ukitarajiwa kubadilika ama kubaki hivyo hivyo baada ya mchezo wa mwishoni wa Kundi hilo kati ya Simba SC dhidi ya APR ya Rwanda.
Singida FG na Simba kila moja ina pointi sita lakini zinatofautiana mabao ya kufunga na kufungwa, huku APR ikiwa ya tatu.
Katika mchezo dhidi ya Simba SC uliopigwa juzi Jumatano (Januari 03), Kyombo alikutana na kikosi chake zamani kwa mara ya kwanza tangu aliptolewa kwa mkopo kwenda Singida na aliupiga mwingi akiwa mmoja ya washambuliaji walioisumbua sana ngome ya Simba SC kwa dakika 90 za mchezo huo.