Mabingwa wa Soka nchini Hispania Fc Barcelona wamemsajili mchezaji mpya Vitor Roque mwenye umri wa miaka 18, kwa wakati na jana Alhamisi alitarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Las Palmas.
Barca walipata uhamisho wa Roque kutoka Athletico Paranaense Julai, mwaka jana kwa mkataba wa thamani ya zaidi ya euro milioni 60.
Kuwasili kwake Hispania hakukupangwa hadi mwanzoni mwa msimu wa 2024/25 huku kukiwa na vizuizi vya matumizi, lakini muda huo ulirudisha nyuma Januari hii.
Roque alitambulishwa na klabu yake mpya mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, lakini uvumi mapema juma hili ulidai Barca inaweza kusajili uhamisho huo na LaLiga.
Xavi alionyesha matumaini alipozungumza na vyombo vya habari, huku usajili huo ukipewa mwanga wa kijani saa chache baadae.
Roque alitumia msimu wa 2023 akiwa na klabu yake ya Athletico nchini Brazil akicheza kama namba tisa, akifunga mabao 21 katika mashindano yote.
Lakini imezua shaka juu ya jukumu atakalokuwa nalo Hispania ikizingatiwa Mshambuliaji Robert Lewandowski yupo na anatumika katika mfumo wa 4-3-3.
Lakini Xavi anaonekana kujiamini wawili hao wanaweza kucheza pamoja, akitoa wito kwa Roque kuwa na uwezo wa kucheza kama mshambuliaji na kutoa Ushindani kwa washambuliaji wote kwenye kikosi.
“Anaweza kucheza na (Lewandowski) kikamilifu,” bosi huyo alisisitiza.
“Anaweza kucheza nje au kama namba tisa. Atazalisha ushindani kwa washambuliaji wote katika kikosi Lewandowski, Ferran (Torres), Joao (Felix), Raphinha na Lamine (Yamal).
“Tutashughulikia mambo yake hatua kwa hatua. Yeye ni mtoto mwenye umri wa miaka 18, kwa hivyo hatuwezi kumpa jukumu kwa sasa kwa sababu anahitaji muda wa kuzoea.
“Lakini yuko tayari kucheza na kufanya mazoezi vizuri. Ni mtaalamu na haraka kukabiliana na mazingira yake mapya, lakini tutakuwa waangalifu.”