Klabu ya Man Utd imepanga kuchinja nyota wao watano kuanzia dirisha la usajili la Januari, 2024 na lile kubwa ili kupata fedha za kushusha majembe mengine.

Hii inakuja siku chache baada ya tajiri Sir Jim Ratcliffe kukamilisha ununuzi wa hisa zake kwa asilimia 25, na sasa yuko tayari kwa usimamizi na uendeshaji kikosini hapo.

Bilionea huyo wa Uingereza ana nia ya kubadilisha muundo wa usajili wa United na kuondokana na porojo za gharama kubwa zilizokuwa zikifanywa na utawala wa zamani.

Tayari United imewaruhusu Donny van de Beek kutua Eintracht Frankfurt kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huku, Sergio Reguilon akikatishiwa mkataba wake na kurejea Tottenham baada ya kudumu kwa minne Old Trafford.

Kocha wa Man United, Erik ten Hag anatazamiwa kuendelea kuwaruhusu nyota wengine zaidi kwenye usajili huu wa dirisha dogo.

Nyota walio njiani kuondoka kuanzia dirisha hili na lile kubwa ni Jadon Sancho ambaye anatarajia kwenda kwa mkopo Borussia Dortmund, Anthony Martial mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu na Ten Hag hana mpango Casemiro ambaye kiwango chake kimeshuka, sasa United wanasubiri ofa kubwa kutoka klabu za Saudi Arabia.

Raphael Varane ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu na amegoma kuongeza tena naye ataondoka.

Sofyan Amrabat pia anatajwa kuwa atarudishwa Fiorentina baada ya kushindwa kuonyesha uwezo wake, akiwa United kwa mkopo.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 6, 2024
Kinda la Kibrazil tishio FC Barcelona