Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi amefurahishwa na viwango bora vya wachezaji wake vijana aliowapandisha katika msimu akiwemo beki wa kati, Hamis Nanguka akiamini ndio mrithi wa mabeki wake, Ibrahim Bacca na Dickson Job.
Nyota huyo amepandishwa katika msimu huu baada ya Gamondi kufurahishwa na kiwango chake kabla ya kumuamini na kumpandisha katika kikosi cha wakubwa.
Beki huyo juzi Alhamis (Januari 04) aliibuka Mchezaji Bora wa mchezo wa Kombe la Mapinduzi waliocheza dhidi ya KVZ kwenye Uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar.
Gamondi amesema kuwa yeye muumini wa wachezaji vijana, hivyo amepanga kuendelea kunitumia beki huyo mwenye uwezo wa kucheza kiungo mkabaji namba sita katika Ligi Kuu Bara na michuano mengine.
Gamondi amesema kuwa anataka kuona beki huyo akiendelea kukua kadiri siku zinavyokwenda ili kuhakikisha anatimiza ndoto zake.
Ameongeza kuwa anafurahishwa zaidi na beki huyo kutokana kucheza kwa kufuata maelekezo yake kuanzisha mashambulizi kuanzia chini golini kwao kwenda kwa wapinzani.
“Hamis ni kati wachezaji ninaowandaa kwa ajili ya baadae, hivi sasa anapata uzoefu huku akiendelea kujifunza kwa wakubwa zake aliowakuta.
“Namtaka aendelee kufuata miiko ya soka ili kufikia malengo yake, ninaamini kiwango bora ambacho anacho hivi sasa ambacho kinanishawishi kuendelea kumtumia katika ligi na mashindano mengine,”‘amesema Gamondi.