Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya – NHIF, umekanusha taarifa za upotoshaji zinazosambaa kwenye Mitandao ya kijamii zikielezea kuzuiwa kwa kadi za Wanachama
Kupitia taarifa iliyotolewa hii leo Januari 7, 2024 na Kaimu Meneja Mawasiliano wa Mfuko huo, Grace Michael, imeeleza kuwa taarifa hizo ni zile zinadoda kuna zuio la kupata huduma ama kupewa rufaa kwenye hospitali za binafsi zilizosajiliwa na Mfuko.
“Taarifa hizi hazina ukweli wowote na badala yake zina nia ovu ya kuleta taharuki kwa wanachama wa Mfuko. Ukweli ni kwamba huduma za matibabu kwa wanachama wakezinaendelea kama kawaida kupitia vituo zaidi ya 9,000 vilivyosajiliwa na Mfuko,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarufa hiyo imezidi kufafanua kuwa, huduma hizo zinaendelea kutolewa ikiwa ni pamoja na Vituo vya Binafsi, Madhehebu ya Dini na Serikali.
Aidha, kutokana na tukio hilo, mfuko umewahakikishia wanachama wake kuwa huduma za matibabu zinaendelea kama kawaida katika Vituo vyote vilivyosajiliwa na Mfuko na endapo kutakuwa na mabadiliko yoyote taarifa rasmi itatolewa kupitia njia rasmiikiwemo kurasa za Mfuko zilizoko kwenye mitandao ya kijamii.
Imeeleza kwamba endapo mwanachama atakutana na changamoto ya kukataliwa huduma katika kituo cha huduma atoe taarifa kupitia ofisi za Mfuko zilizo karibu au kupiga simu namba 199.