Klabu ya Singida Fountain Gate imekiri kwamba bado inakumbuka makali ya kiungo wake Mbrazili Bruno Gomes ambaye anaendelea kukosa mechi zao kutokana na majeraha.

Kocha msaidizi wa Singida, Nizar Khalfan amesema kikosi chao kuendelea kumkosa Gomes ni pengo kubwa ingawa maisha yao yanaendelea kwa kuwatumia wachezaji wengine.

Nizar amesema Gomes ni kiungo fundi ambapo klabu yao inaendelea kupambana kumtafutia tiba ya muda mrefu kufuatia kila wakati kuwa majeruhi akirudishwa jijini Dar es salaam.

“Kwenye mechi kubwa unahitaji wachezaji washindani, tunao wengi na mmoja wao ni Bruno (Gomes) wote tunajua ubora wake na jinsi alivyo jasiri kufanya uamuzi mkubwa,” amesema

Tunaendelea kumkosa kutokana na kuwa majeruhi, uongozi unasaidiana naye ili arudi haraka uwanjani kuendelea na majukumu yake. Maisha lazima yaendelee tunaendelea kuwapa nafasi wachezaji wengine kwenye kikosi.”

DC Sima awa mbogo mahudhurio hafifu Kidato cha kwanza
Riyad Mahrez : Tunajua maana ya AFCON