Jumuiya ya Kampuni za Kuongoza Uwindaji wa Kitalii Nchini -TAHOA, imeendelea kutoa mkono wa pole kwa jamii ya Wana Hanang’ waliopatwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Desemba, 2023 kwa kukabidhi mabati 1,143 ikiwa ni mchango wa vifaa vya ujenzi.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo hii leo Januari 11, 2024 Wilayani Hanang Mkoani Manyara, Katibu Mkuu wa TAHOA, Suleiman Masato amesema kuwa wameguswa na maafa hayo, huku ikiahidi kuendelea kutoa michango mbalimbali, ili kusaidia Waathiriwa.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja ameishukuru TAHOA kwa kuguswa na matatizo yaliyotokea Wilayani Hanang na kwa kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MheDkt. Samia Suluhu Hassan za kuwajengea makazi bora Wananchi wa Hanang.

“Mchango huu mliouleta umegusa maisha ya Wananchi wa Hanang waliopata madhara ya mafuriko kama tunavyojua wengine wamepoteza makazi na vifaa mbalimbali na nafahamu mlitanguliza kutoa mchango wa fedha katika akaunti ya maafa lakini leo mmekuja kwa mara nyingine hapa Hanang kwa ajili ya kuleta vifaa vya ujenzi, hivyo kwa niaba ya Serikali nawashukuru sana,” amesema Mayanja.

Mchango huo wa mabati, unakuja ikiwa ni mwendelezo wa TAHOA kutoa mkono wa pole kwa Wana Hanang ambapo awali ilichangisha Shilingi 47 milioni na kuzikabidhi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama.

Gift Fred atangaza njaa Young Africans
DC Sima awa mbogo mahudhurio hafifu Kidato cha kwanza