Polisi Mkoani Manyara, inawashikilia watu 21 kwa tuhuma za kujihusisha na uhalifu wa makosa ya kimtandao, ikiwemo kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara, Kamishna Msaidizi wa Polisi, George Katabazi  ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kudai kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika kipindi cha kuanzia Desemba 2023.

Amesema, watuhumiwa hao wamekutwa na vielelezo mbalimbali ikiwemo mavazi ya wakala wa watoa huduma za simu, line za simu zilizobatilishwa 32, simu za kiganjani 98 na fedha kiasi cha Shilingi 44 Milioni, zilizokuwa zimeibwa.

Kufuatia matukik hayo, Katabazi amewataka Wananchi kuchukua tahadhari kwa kuacha tabia ya kuwaamini wahalifu wanao walaghai kwa kupata nafuu ya riba wa mkopo au pembejeo mtandaoni, kwani ni waongo na hutumia mwanya huo kujipatia kipato isivyo halali.

 

Imani potofu yahusishwa tukio la mauaji Makete
Mauaji yasababisha Burundi kuitenga Rwanda