Wananchi wa Iwawa wilayani Makete Mkoa wa Njombe, wametakiwa kuacha kufanya matukio ya mauaji ambayo yamekuwa yakileta taharuki kwa jamii kwa imani za kishirikina.

Wito huo, umetolewa naKamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mahamoud Banga wakati akitoa pole kwa wafiwa ambao ndugu yao aliuawa kwa kukatwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili.

Amesema, Wananchi na wanandugu wanatakiwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi, ili hatua stahiki zichuliwe dhidi ya watekelezaji wa tukio hilo, ili kutokomeza matukio kama hayo katika jamii.

Aidha, Kamanda Banga pia amewaasa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, ambavyo mara nyingi vimekuwa vikitokea lakini baadhi wamekuwa wakificha, kiyu ambacho si sahihi na kuwataka washirikiane na Polisi kutokomeza uhalifu.

 

300 wapoteza maisha kwa mafuriko Kongo
Polisi yawadaka 21 kwa uhalifu wa mtandao