Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilayani Nachingwea, imemukumu kwenda jela miaka 30 Shaibu Makunda (38), maarufu kwa jina la Makompyuta kwa kupatikana na hatia ya ubakaji.

Makompyuta ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mtua Wilayani humo, alipewa hukumu hiyo Januari 11, 2024 na alikuwa akituhumiwa kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 17.

Mbele ya Mahakama, ilidaiwa kuwa mtuhumiwa huyo Shaibu alitenda kosa hilo Machi 19, 2023 kijijini hapo na baadaye alikamatwa na raia wema ambao hawakufurahishwa na tukio hilo.

Akitoa hukumu hiyo ya kesi namba 08 ya mwaka 2023 Hakimu Mkazi, Neema Mhelela alisema Mahakama imejiridhisha pasi na shaka baada ya kusikiliza mashahidi watano upande wa Jamhuri na hivyo kumtia hatiani mtuhumiwa huyo.

Wananchi wapongeza huduma Mama Samia Legal Aid
Hofu yatanda ongezeko Watoto wenye Ulemavu