Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa mashtaka ya umma DPP, imeamuru kushtakiwa mara moja kwa mshukiwa mkuu wa mauaji ya Shakahola, Paul Mackenzie na wenzake 94, kwa tuhuma za mauaji, kushambulia na kusababisha madhara ya mwili, kujihusisha na uhalifu wa kupangwa, kutesa watoto na kuwanyima haki za kimsingi.

Mapema hivi karibuni, Mahakama ya Shanzu ya Nchini Kenya ilikuwa ikifikiria kumuachilia kwa dhamana mshukiwa huyo na wenzake, iwapo Serikali itashindwa kuwafungulia mashtaka.

Mahakama hiyo, hata hivyo ilisema imeamua Mackenzie na washukiwa wenzake hao kuendelea kuzuiliwa kwa siku 14 zaidi, ili kutoa muda kwa Serikali kuchukua hatua.

Hatua hizo ni pamoja na kuwafunguliwa mashtaka watuhumiwa hao au iwaachiliwe kwa dhamana hadi pale upande wa mashtaka utakapokuwa tayari kufanya hivyo kitu ambacho kimetekelezwa.

Hii hapa Rekodi ya Pa Omar Jobe
Ajax yajitosa usajili wa Henderson