Mahakama Kuu ya Malindi Nchini Kenya, imetoa amri kuwa Muhubiri tata Paul Mackenzie na washukiwa wengine 31 wafanyiwe uchunguzi wa akili na afya zao kwa jumla, kabla ya kesi ya mauaji dhidi yao haijaanza kusikilizwa rasmi.

Akitoa amri hiyo, Jaji wa Mahakama hiyo, Mugure Thande amesema zoezi hilo linapaswa kufanyika ndani ya siku 14 toka tarehe ya amri hiyo, kutokana na ombi la upande wa mashtaka.

Mapema wiki hii, Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa mashtaka ya umma DPP, iliamuru kushtakiwa mara moja kwa mshukiwa huyo Mackenzie na wenzake, kwa tuhuma za mauaji, kushambulia na kusababisha madhara ya mwili, kujihusisha na uhalifu wa kupangwa, kutesa watoto na kuwanyima haki za kimsingi.

Hatua ya kuwashitaki washukiwa hao, ilitokana na Mahakama ya Shanzu kufikiria kumuachilia kwa dhamana mshukiwa huyo na wenzake iwapo Serikali itashindwa kuwafungulia mashtaka.

PAC wachambua taarifa ya ukaguzi huduma za afya
Iwobi aichimba mkwara Ivory Coast - AFCON 2023