Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), chini ya Mwenyekiti wake Naghenjwa Kaboyoka imepitia na kuchambua taarifa ya ukaguzi wa ufanisi katika udhibiti wa utoaji wa huduma za afya kwenye vituo binafsi na vya hiari.
Kamati hiyo, pia imepitia na kuchambua taarifa ya ukaguzi wa kiufundi kuhusu ujenzi wa Shule za Sekondari kupitia mradi wa kuboresha elimu ya sekondari (SEQUIP).
Kikao hicho kimefanyika hii leo Januari 17, 2024 katika kumbi za Bunge jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila.

Vita ya majirani - AFCON 2023
Mahakama yaamuru Mhubiri Mackenzie apimwe akili