Shirika la Reli Tanzania – TRC, limeutaarifu Umma kuwa limesitisha kwa muda huduma ya safari za treni kutoka Dar es Salaam kuelekea Mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Katavi, Kigoma, Shinyanga na Mwanza, pamoja na mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Jarnila Mbarouk imeeleza kuwa hatua hiyo inatokana na uharibifu wa Miundombinu ya Reli katika maeneo ya Mazimbu, Kilosa na Munisagara Mkoani Morogoro, Godegode na Gulwe Mkoani Dodoma.

Maeneo mengine ni Ruvu junction, Wami, Mvave mkoani Pwani, eneo la Mkalamo Tanga kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, huku ikiarifiwa kuwa Wahandisi kutoka TRC wanaendelea na matengenezo katika maeneo yaliyoathiriwa na mvua zinazoendelea.

Aidha, huduma hizo za usafiri wa treni zinatarajia kuanza Januari 23, 2024 katika Reli ya kati na kuelekea Mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro na Arusha), baada ya kukamilika uimarishaji wa miundombinu.

Aidha, TRC inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na inawasihi wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi cha matengenezo iii kuhakikisha usafiri unarejea katika hali ya usalama.

Karim Benzema amshitaki waziri Ufaransa
Nigeria haitaki kurudia makosa - AFCON 2023