Afisa mmoja wa Polisi amefariki na wengine wawili kujeruhiwa baada ya bomu la kutengeneza kwa mkono lililokuwa limefungwa kwenye toroli linalokokotwa na Punda, kulipuka kwenye mpaka kati ya Mandera na Bula Hawa kaunti ya Mandera Nchini Kenya.

Tukio hilo la lililotokea hii leo Januari 18, 2024, lilitokea wakati Punda wawili waliokuwa wakivuka na mizigo kutoka upande wa Nchi ya Somalia kuwakaribia Polisi hao na ndipo kilipuzi kilipodondoka na kuleta madhara hayo.

Hata hivyo, Polisi imesema washukiwa wa tukio hilo ni kundi la kigaidi Al-Shabaab lililopo kwenye mpaka wa Mandera huku Mshirikishi Mkuu wa ukanda wa Kaskazini Mashariki, John Otieno akithibitisha kifo hicho.

Maafisa wanaosimamia mpaka huo walikuwa wamewasimamisha wanyama hao kwa ukaguzi wa kawaida wa bidhaa na nyaraka nyingine zinazohitajika wakati mkokoteni huo ulipowasili, ambapo mashuhuda walisema mlipuko huo ulisababisha moto mkubwa katika eneo la tukio na Punda hao walijeruhiwa.

Mashabiki Ghana watofautiana - AFCON 2023
Okocha: Nigeria tuna nafasi kubwa AFCON 2023