Mbunge wa jimbo la Hanang’, Samwel Hayyuma amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumchagua Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na Dar24 Media Jijini Dodoma Hayyuma amesema Dtk. Samia anajicho la kuona mbali na kwa mtazamo wake amefanikiwa kumteua Nchimbi kushika nafasi hiyo.

Amesema, “kwanza kwa Chama cha mapinduzi tunaakiba ya kutosha ya vyuma vya kutosha tena ambavyo vimeiva, na ukiangalia kwa Dkt. Nchimbi ni moja kati ya zao la mapinduzi kutoka chini,na alishawai kuwa Mwenyekiti wa Vijana.”

Hata hivyo, amesema katika kuelekea uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, ni wazi kuwa Dtk. Nchimbi ndio atakisaidia chama kutokana na uzoefu wa siasa tangu akiwa chipukizi mpaka sasa.

Wapya Simba SC wapewa masharti mazito
DC Malisa awaonya vikali wanohujumu mpango wa Rais