Ofisa Mtendaji Mkuu wa lhefu, Olebile Sikwane amesema baada ya kukabidhiwa wadhifa huo, malengo yao mapya ni kuhakikisha kikosi hicho cha jijini Mbeya kinasalia katika Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao kisha mipango mingine itafuata.

Sikwane aliyekabidhiwa nafasi hiyo aliyokuwa anaitumikia pia akiwa na Singida Fountain Gate, amesema mipango yao ni ya muda nfupi ingawa kuanzia msimu ujao mambo yatakuwa mazuri zaidi hivyo kikubwa anachoomba ni sapoti tu ya mashabiki wao.

“Kitu kizuri ni kwamba nafanya kazi niliyotoka kuifanya katika klabu nyingine, hivyo kwangu ni nafasi ya kuonyesha tena na kuendeleza uwezo wangu, naamini kwa ushirikiano uliopo baina yetu tutapiga hatua kubwa kiushindani nchini, amesema.

Raia huyo wa Botswana ameongeza kuwa, jambo linalompa matumaini ya kufanya vizuri kama ilivyokuwa Singida ni uwepo wa baadhi ya watendaji wengine walioongozana naye katika maisha hayo mapya hivyo kwake anaona uwezo wao wa kifikra utaleta tija.

Baadhi ya watendaji waliojiunga na Sikwane ni aliyekuwa kocha msaidizi wa Singida FG Mathias Lule na Mkurugenzi wa Ufundi, Ramadhan Nswanzurimo.

Wabunge wa CCM washindwa kuzuia hisia zao
Benchikha kuzivutia kasi Azam, Young Africans