Kocha Mkuu wa Zambia, Avram Grant amesema wameweka kando matokeo ya sare walioyapata katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kuweka mkazo kwenye mchezo wao unaofuata dhidi ya Tanzania.

Kocha huyo mkongwe aliona hakuna sababu ya kufikiria matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya DRC kwenye mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Mataifa ya Afrika lakini kuweka mkakati mpya wa mechi yao inafuata.

“Kila mechi ni tofauti na inayofuata itakuwa tofauti na hii. Hakika tutatumia mbinu nyingine kupata ushindi dhidi ya Tanzania,” alisema.

Akizungumza kuhusu kuruhusu bao la kusawazisha la DRC Grant alisema: “Ilikuwa mechi ngumu kwa kila timu. Nafikiri tulicheza vizuri. Tulifunga lakini haraka wakasawazisha.

“Niligundua DRC walikuwa bora kuliko sisi, lakini tulizuia vizuri na timu yangu ilipambana vizuni,” amesema Grant.

Grant pia alizungumzia ugumu wa wachezaji wake kupata upana kwenye mechi hiyo.

“Tulisukuma mashambulizi ingawaje nilipenda kumiliki zaidi mpira.

“Ilikuwa ngumu kwa washambuliaji wetu. Walifanya kadri ya uwezo wao, lakini wapinzani walikuwa na maumbo makubwa na mabeki wazuri.

Tulicheza kama timu na hicho ndicho ninachotaka kukumbuka,” alisema.

Huduma za Mawasiliano kuboreshwa Hanang'
Kalvin Phillips atajwa tena vita ya usajili