Serikali Nchini, imeandaa minara zaidi ya 30 ambayo itasaidia kupunguza changamoto ya mawasiliano katika Kata ya Gendambi iliyopo Wilayani Hanang’ ambayo ilikumbwa na maafa ya mafuriko na maeneo mengine ya Mkoa wa Manyara.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye wakati alipotembelea eneo la Gendambi Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, lililoathirika na Maporomoko ya Mawe na Matope.
Amesema, pia amatoa pongezi kwa Waandishi wa Habari kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kipindi chote cha maafa, na kudai kuwa Vyombo vya Habari vimefanya kazi kubwa kwa kipindi chote ambacho Wilaya ya Hanang ilikumbwa na maafa hayo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Gendambi, Daniel Hando ameishukuru Wizara hiyo kwa kuahidi kutatua changamoto ya Mawasiliano ambayo imekuwa ikikwamisha shughuli za kimaendeleo na maisha ya kawaida.