Menejimenti ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania – GST, imetakiwa kuongeza juhudi, weledi na ubunifu kwenye utendaji kazi wake, ili kutekeleza agenda ya Vision 2030 kwa ufanisi.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya GST, Prof. Justinian Ikingura katika Kikao cha 17 cha Bodi kilichofanyika hii leo Januari 19, 2024 Jijini Dodoma ambapo pia alipokea taarifa ya Utekelezaji ya GST kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 pamoja na Rasimu ya Bajeti ya Taasisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2024/25.

Kwa upande wake, Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Mussa Budeba amempongeza Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi hiyo kwa maelekezo yao mazuri na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo na ushauri wote uliotolewa na Bodi hiyo.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Budeba amesema GST imeandaa vipaumbele sita kwa lengo la kufanikisha mpango wa utekelezaji wa Vision 2030 ikiwa ni pamoja na kuongeza wigo wa upatikanaji wa taarifa za kina za Jiofizikia kwa kurusha Ndege kutoka asilimia 16 ya sasa hadi asilimia 50 ifikapo Mwaka 2030.

Katika kikao hicho, pia Prof. Ikingura pia alipokea Taarifa ya Kamati ya Fedha na Utawala, Taarifa ya Kamati ya Jiosayansi na Taarifa ya Kamati ya Ukaguzi na kilihudhuriwa na Wajumbe wa Bodi hiyo akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Jiosayansi Dkt. Dalaly Kafumu, Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi, Bertha Sambo, Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Utawala, CPA Constantine Mashoko pamoja na Menejimenti ya GST.

Ivan Toney: Nitaondoka Brentford
Ushushaji gharama za uletaji wa Mafuta kuleta ahueni - Dkt. Biteko