Serikali Nchini, imedhamiria kuimarisha na kuwekeza kwenye Afya za vijana balehe hasa katika hali za Lishe, Afya ya Akili pamoja na elimu, ili kujikinga na magongwa yakuambukiza ikiwemo VVU/UKIMWI ikiwa ni kipaumbele cha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema hayo wakati akifungua Kongamano la Tano la Kisayansi kuhusu masuala ya vijana balehe lenye lengo la kujadili namna ya kubadili Tafiti za Afya kwa Vijana wa rika balehe na Lishe kuwa za vitendo.

Amesema, “Vijana hawa balehe wana changamoto nyingi ikiwemo ya masuala ya lishe, Afya ya Uzazi, Afya ya Akili, lakini pia vijana wengi wanakabiliwa na upungufu wa damu kwa asilimia 38-40, uzito mkubwa, uzito mdogo pamoja na ukosefu wa vitamini.”

Waziri Ummy ameongeza kuwa kuzinduliwa kwa utafiti katika Kongamano hilo pia kutasaidia wakina mama wajawazito kupewa madini ya ‘calcium’ ili kuwa na uwezekano wa kupunguza kifafa cha mimba kinachochangia vifo vya kina mama wajawazito.

Amesema, utafiti huo umeonesha badala ya kuwapa dozi ya Mg 1,500 kwa siku hata wakipewa dozi ya Mg 500 kwa siku inaweza kusaidia matokeo mazuri kwa kinamama wajawazito kutopata kifafa cha mimba ambapo pia itapumguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga.

Uendeshaji Halmashauri Serikali za Mitaa wajadiliwa
Shetani afikishwa Mahakamani kwa mauaji Sengerema