Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, imepokea na kujadili taarifa ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, kuhusu usimamizi na uendeshaji wa Sekretarieti za Mikoa: Mafanikio, Changamoto na hatua za utatuzi.

Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wake, Denis Londo pia kimepokea na kujadili taarifa ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuhusu usimamizi na uendeshaji wa Halmashauri za Serikali za Mitaa: Mafanikio, Changamoto na Hatua za utatuzi.

Aidha, Kamati pia ilipokea na kujadili taarifa ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuhusu usimamizi wa shughuli za ujenzi wa miundo ya barabara wa kawaida na wakati wa dharura, chini ya mamlaka za serikali za mitaa.

Kikao hichon kilifanyika  katika kumbi za Bunge jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Adolf Ndunguru na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila.

Makala: Ya Bodaboda Polisi wasiangushiwe jumba bovu
Vijana Balehe kuimarishiwa hali ya lishe