Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kilindi, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Kasikana amewataka Viongozi, Wananchi na Jamii ya Kimasai wa Kitongoji cha Matangagonja Kijiji na Kata ya Kilindi Asilia, Tarafa ya Kimbe Wilayani humo Mkoani Tanga kufuata imani zao kwa kuheshimu katiba ya nchi, ili kudumisha amani.

Kasikana ameyasema hayo wakati akitoa elimubkwao na kudai kuwa kila mtu anayo haki ya kuabudu na kuamini anachoona kinafaa lakini hatakiwi kuvunja sheria za nchi kama ilivyoelekezwa kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,  hivyo kumpangia mtu cha kuamini au kuabudu ni kinyume na katiba ya Nchi.

Amesema Wananchi hao wanatakiwa kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na kwamba wale wanaoamini na wasioamini  katika mila wanatakiwa kuacha kujichukulia sheria mkononi na kuwasihi endapo kuna tatizo au changamoto yoyote wanayokutana nayo watoe taarifa mapema, ili iweze kufanyiwa kazi.

Jeshi la Polisi Nchini limeendelea na harakati zake za utoaji elimu kwa rika na maeneo mbalimbali, likilenga kupunguza na kuondosha kabisa vitendo vya kihalifu.

Jenerali Mkunda akubali kasi Ujenzi Nyumba 5,000 Msomera
Nchimbi aanza kazi kwa mambo matatu CCM