Uongozi wa Simba SC umeweka wazi sababu kubwa ya kuachana na na wachezaji wao wawili Jean Baleke na Moses Phiri, huku wakisema kuwa kocha hakuwahitaji wachezaji hao na badala yake aliomba wasajiliwe washambuliaji wengine.

Nafasi za Baleke na Phiri zimechukuliwa na washambuliaji wengine wawili wa kigeni ambaoni Pah Jobe na Fredy Michael Kouablan.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema: “Watu wamekuwa wakilalamika haswa mashabiki wa Simba SC kuwa kwanini tumewaacha Baleke na Phiri kwa nini tumewaacha, ngoja niwaambie kitu kuwa sisi tunafanya vitu kwa kufuata benchi la ufundi.

Yale yalikuwa ni maamuzi ya benchi la ufundi kuhakikisha kuwa wanaunda timu bora, benchi la ufundi ndio waliomba ufanyike usajili wa wachezaji wawaili wa ushambuliaji na sisi tukatekeleza.

Kama wachezaji wanakosa nidhamu basi wanakuwa moja kwa moja wanakosa sifa ya kuwa sehemu ya kikosi chetu, hawa washambuliaji waliokuja leo hii ndani ya samba SC, nawahakikishia kuwa mtafurahi,” amesema Ahmed.

Manchester City yashtukia jambo
Kocha Senegal yupo salama